Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Wabunge wa Ukraine lachapana makonde. Spika apigwa na mayai. Wasambaratishwa na gesi ya machozi

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter Wanamaji wa Urusi sio tatizo Ukraine- bunge hatimaye lapitisha mswada




Manuwari za jeshi la wanamaji la Urusi
Ukraine imewaruhusu wanamaji wa Urusi kuendelea na shughuli zao Crimea


Bunge la Ukraine limepitisha hatua ya Urusi kuendelea na shughuli zake katika kituo cha jeshi la wanamaji cha Crimea, katika maji ya Black Sea.
Hata hivyo kulikuwa na fujo bungeni wakati wa majadiliano kuhusu hatua hiyo.
Wabunge walipigana, huku Spika akijificha chini ya mwavuli, wakati wabunge walikuwa wakimpiga kwa mayai.
Mabomu yanayotoa moshi pia yalitegwa nje ya bunge.
Nje ya bunge, polisi walipambana na maelfu ya waandamanaji, wengine wakiunga au kupinga makubaliano ya wiki iliyopita kati ya marais wa Ukraine na Urusi ya kuongoza muda zaidi katika Urusi kukimiliki kituo hicho cha kijeshi.


Tags:

0 comments

Post a Comment