IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
WASHINGTON:
Syria na Iran zimetuhumiwa na Marekani na Israel kuwa zinatoa msaada wa silaha kwa wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon. Waziri wa Ulinzi wa Marekani Robert Gates amesema, miongoni mwa silaha hizo ni makombora ya kisasa. Hiyo inaweza kuvuruga usalama katika kanda hiyo ya Mashariki ya Kati aliongezea waziri Gates baada ya kukutana na waziri mwenzake wa Israel Ehud Barak mjini Washington.
Kwa upande wake Barak amesema, Israel haitaki kuchochea mapambano yo yote, lakini serikali yake ipo macho. Katika mwaka 2006, majeshi ya Israel yalifanya mashambulio dhidi ya Hezbollah nchini Lebanon. Si chini ya watu 1,200 waliuawa upande wa Lebanon, wengi wao walikuwa raia wa kawaida. Israeli nayo ilipoteza watu 160 wengi wao walikuwa wanajeshi.
You Are Here: Home - - Syria na Iran zatuhumiwa kuwapatia silaha Hezbollah nchini Lebanon
0 comments