Mdahalo huo ulionyeshwa moja kwa moja kupitia televisheni.
Waziri mkuu Gordon Brown, na wapinzani wake, David Cameron wa chama cha Conservative na Nick Clegg wa Liberal Democrats, walijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na watu walioalikwa kwenye mdahalo huo.
Maswali hayo yalihusu mada mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhamiaji na namna ya kutatua suala la nakisi ya bajeti ya Uingereza.
Midahalo mingine miwili ya televisheni ikilenga masuala ya nje na uchumi wa Uingereza, imeandaliwa kufanyika kabla ya siku ya uchaguzi , tarehe sita Mei mwaka huu.
Maoni ya haraka baada ya mdahalo huo yamempa ushindi bwana Clegg ambaye chama chake kinaweza kuleta uwiano katika uongozi wa nchi hiyo baada ya uchaguzi.

0 comments