Baraza jipya la mawaziri nchini Nigeria, linatarajiwa kuapishwa hii leo katika hafla itakayoongozwa na kaimu rais wa nchi hiyo Goodluck Jonathan.
Mawaziri 38 walioteuliwa na Bwana Jonathan wiki iliopita, waliidhinishwa na bunge la Senate nchini humo. Mawaziri hao wanatarajiwa kuhudumu hadi mwaka ujao wakati uchaguzi mkuu utakapofanyika.
Baraza hilo la mawaziri linajumuisha mfanyabiashara mmoja kutoka Marekani na mshauri wa masuala ya kiuchumi katika benki ya uwekezaji ya Goldman Sachs, Olusegun Aganga.
Mawaziri wengine waliokuwa wakihudumu kwenye baraza lililovunjwa akiwemo mpwa wa rais anayeugua Umaru Yar'Adua, ni miongoni mwa walioteuliwa kwenye baraza hilo.
Wadadisi wa siasa wanasema uteuzi huo unaashiria juhudi za Bwana Jonathan za kujiimarisha kisiasa.
0 comments