Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Tume mbili muhimu zazinduliwa Zimbabwe

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Tume ya kwanza ya kutetea haki za binadamu na ya uchaguzi nchini Zimbabwe zimezinduliwa rasmi na Rais Robert Mugabe.
Kuundwa kwa tume hizo mbili kunaonekana hatua muhimu katika kuwezesha kuwepo uchaguzi wa huru na wa haki.
Hatua hii ni miongoni mwa utekelezaji wa makubaliano ya kugawana madaraka baina ya Bw Mugabe na waziri mkuu Morgan Tsvangirai, ingawa masuala mengine bado hayajafanyiwa kazi.
Mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu atakuwa Reginald Austin, Profesa wa masuala ya sheria na alikuwa kiongozi wa kitengo cha sheria cha jumuiya ya madola.
Mkuu wa tume ya uchaguzi atakuwa aliyekuwa jaji wa mahakama kuu wa nchi hiyo, Simpson Mutambanengwe, ambaye alikuwa akifanya kazi kama kaimu mkuu wa sheria katika mahakama kuu ya Namibia.
Tags:

0 comments

Post a Comment