Shinikizo zimeendelea kuwepo dhidi ya Israel za kuitaka itoe maelezo kuhusu kutumiwa kwa pasipoti za ulaya na watu wanaoshukiwa kumwuua mwanamgambo mmoja wa Palestina nchini Dubai mwezi uliopita.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Miliband amesema serikali ya Uingereza inatarajia Israel kutoa ushirikiano katika uchunguzi wa kesi hiyo, baada ya maafisa wa serikali ya Uingereza kukutana na balozi wa Israel kwenye ofisi ya mambo ya nje kuelezea wasi wasi wao.
Ufaransa na Ireland pia zimechukua hatua sawa na hiyo ya Uingereza.
Bwana Miliband amesema hangependa nchi zingine ulimwenguni kupoteza imani na paspoti za Uingereza.
Amesema pasipoti zilizotumika katika tukio hili hazikuwa na teknolojia mpya ya sasa inayotumia chipu ya kuhakikisha kwamba hazitumiki vibaya.
0 comments