Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Jeshi lafanya mapinduzi Niger

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Rais wa Niger aliyepinduliwa, Mamadou Tandja.
Rais wa Niger aliyepinduliwa, Mamadou Tandja.Kikosi cha jeshi nchini Niger kimethibitisha kufanya 

Baada ya mapinduzi hayo, utawala wa kijeshi ukaivunja serikali


mapinduzi nchini humo na kutangaza kuwa kimeivunja serikali ya nchi hiyo. Tangu jana Rais wa Niger Mamadou Tandja na baraza lake la mawaziri wanazuiliwa na wanajeshi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Niamey. Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi-ECOWAS, zimelaani mapinduzi hayo ya kijeshi.
Mvutano wa kisiasa umekuwa ukiendelea nchini humo baada ya Rais Tandja mwezi Agosti mwaka uliopita kulivunja bunge na mahakama ya kikatiba akishinikiza katiba ya nchi hiyo ifanyiwe mabadiliko yatakayomuwezesha kuendelea kuwepo madarakani kinyume na katiba, hatua iliyokosolewa ndani na nje ya nchi hiyo.
Tags:

0 comments

Post a Comment