Rais Barack Obama hii leo anatarajiwa kukutana na kiongozi wa kidini wa Tibet Dalai Lama mjini Washington.
Mkutano huu unafanyika huku tofauti zikiibuka kati ya Marekani na mshindani wake wa kiuchumi Uchina.
Nayo serikali ya Beijing imeionya Marekani kuwa iwapo mkutano huu utafanyika basi utaathiri zaidi uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Tayari Uchina umetishia kusitisha mpango wake wa kubadilishana mafunzo ya kijeshi kati yake na Marekani.
0 comments