Serikali ya Gambia imemfukuza mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia watoto nchini humo, Min Whee- Khan.
Bi Whee - Kang amepewa saa 24 kuondoka mjini Banjul. Haijabainika kilichosababisha afisa huyo kufukuzwa kutoka Gambia.
Waandishi wa habari wamesema nchi hiyo imekosolewa vikali dhidi ya rekodi yake ya haki za binadamu.
Wakosoaji wa Rais Yahya Jammeh ambaye alitwaa madaraka kupitia mapinduzi mwaka wa 1994 wamekuwa wakilengwa na maafisa wa usalama mara kwa mara.
Bi Min Whee- Kang ndiye afisa wa tatu wa kimataifa kufukuzwa nchini Gambia chini ya utawala wa Bw. Jammeh.
0 comments