Chama Tawala nchini Tanzania CCM kimeridhia mapendekezo ya kuundwa kwa serikali shirikishi huko Zanzibar kama njia muafaka ya kuondoa chuki.
Kikao hicho kilichomalizika manane za usiku kimetaka kura za maoni kuhusu serikali hiyo zipigwe na Wazanzibari wote kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Malumbano katika chama cha CCM pia yalijadiliwa kwa kina ambapo kikao kiliongezea muda wa mwezi mmoja kamati teule ili juhudi za upatanishi ziendelee kati ya makundi zinazozozana na kupatikana maridhiano.
0 comments