Wataalamu wathibitisha wanja ni dawa | ||||
Utafiti uliofanywa Ufaransa, unapendekeza kuwa wanja unaopakwa machoni kwa kiwango kikubwa ambao ulitumiwa sana enzi za zamani nchini Misri kama Cleopatra huenda zikawa na faida za kitabibu na urembo. Cleopatra alikuwa malkia nchini Misri aliyejulikana sana kwa uzuri wake. Utafiti huo, uliochapishwa katika jarida la Analytical Chemistry, unapendekeza kwamba wanja huo ulisaidia kulinda macho dhidi ya maradhi. Utafiti huo unaonyesha kuwepo na chembechembe za madini ya risasi katika kipodozi hicho. Kwa kiwango kidogo sana, chembechembe hizo hutoa gesi ya nitric, inayoongeza nguvu kwenye mfumo wa kingamaradhi ili kupambana na bakteria inayoweza kusababisha athari kwenye macho. |
You Are Here: Home - - Wataalamu wathibitisha wanja ni dawa
IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
0 comments