Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Obama abeba lawama za usalama

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Obama abeba lawama za usalama
Rais Obama ametangaza matokeo ya uchunguzi ulioendeshwa na ikulu ya Marekani kuhusu dosari za usalama kufuatia jaribio la raia wa Nigeria Umaru Farouk Abdul Mutallab la kuilipua ndege ya Marekani eneo la Detroit siku ya krisimasi.

Bw Obama amesema serikali yake ilikuwa na taarifa muhimu za kuzuia shambulio hilo. Hata hivyo maafisa wa ujasusi walipuuza taarifa hizo na kuhatarisha nchi hiyo.

Rais huyo sasa ametangaza masharti mapya ambapo ameagiza taarifa zote za kiusalama zitolewe kwa vyombo vyote vya serikali.

Obama pia amesema yupo tayari kubeba lawama kosa linapotokea na kuongeza Marekani itaendelea kukabiliana na kundi la Al-Qaeda.

Tags:

0 comments

Post a Comment