Malecela-Mapambano yanaendelea
Ni yule Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tabora Christopher Nyamwanyi, ametangaza nia yake ya kugombea ubunge Jimbo la Mtera kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu. Kwa sasa Jimbo hilo hushikiliwa na Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela. Alisema akima mkoani hapo jana kuwa anakusudia kutumia elimu yake kwa ajili ya wananchi wa Mtera mkoani Dodoma, kwa ajili ya kuwaletea maendeleo. Alisema anataka kutumia haki yake ya kikatibu na kidemokrasia ya kushiriki ndani ya uongozi wa taifa lake, na kwa ajili ya kuwaletea maendeleo pia. "Nataka kutumia haki yangu ya kikatiba na kidemokrasia ya kushiriki katika uongozi wa taifa langu na kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Jimbo la Mtera,” alisema Nyamwanji. Kwani anaamini kuwa yeye ni kijana na ana nguvu na ari ya kufanya kazi na kuwavusha Wanamtera kwenda kwenye maendeleo. Nyamwanji alimalizia kwa kusema kwamba,atashirikiana na wanamtera kubaini fursa zilizopo ili kutumia kutatua matatizo ya kimaendeleo yanayochangia kuwafanya watu wa Mtera wabaki kuwa masikini.
0 comments