Mhubiri wa kiislam aliyefukuzwa kutoka Kenya kutokana na sababu za kuwa tishio kwa usalama, amewasili nchini kwao, Jamaica, ambako amehojiwa na polisi.
Maafisa walisema mhubiri huyo, Abdullah al-Faisal, hakuvunja sheria yeyoye nchini Jamaica, lakini polisi walitaka kujua ni wapi wanaweza kumpata.
Bw al-Faisal, ambaye alitumikia kifungo che jela nchini Uingereza kwa kuchochea mauaji, amaearifiwa kuwafahamisha polisi nchini Jamaica kuwa safari yake ya ndege ya siku mbili kutoka Kenya, iligharimu dola nusu milioni.
Kwa uchache watu watano waliuwawa mjini Nairobi, baada ya polisi kuwafyatulia risasi waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe, ambao walikuwa wanadai kuachiliwa huru kwa Bw al-Faisal.
Serikali ya Kenya ilimkamata Bw al-Faisal mwishoni mwa mwezi uliopita mjini Mombasa kwa madai ya kukiuka kanuni na uhamiaji.
0 comments