MOSCOW
Urusi na Marekani zimesema kuwa zitarejea katika mazungumzo juu ya kufikiwa kwa mkataba mpya wa upunguzaji wa silaha za nyuklia mwanzoni mwa mwezi ujayo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, amesema kuwa umuhimu mkubwa katika mazungumzo hayo utakuwa ni kufikiria masuala machache yaliyobakia kabla ya kusainiwa mkataba huo mpya.
Mpaka sasa mazungumzo hayo yameshindwa kufikia muwafaka wa kuwepo mkataba mpya baada ya ule wa zamani uitwayo START wa kupunguza umilikaji wa silaha za nuklia kati ya mataifa hayo mawili kumalizika mwezi uliyopita.
Rais Barack Obama wa Marekani na mwenzake, Dmitry Medvedev wa Urusi, wote kwa pamoja wamesema kuwa wanataka kuona mkataba mpya unafikiwa.
0 comments