Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA MICHEZO - Mechi za Simba na Yanga kuna nini ndani yake?

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter Kaduguda atoboa siri kubwa
Haruna Moshi 'Boban' wa Simba ambae imedaiwa yupo kwenye orodha mpya ya kocha wa Yanga, Dusan Kondic ingawa duru za ndani ya Simba zinadai kuwa ni ngumu mno mchezaji huyo kung'oka Msimbazi na kwenda Yanga kutokana na wadhamini na washauri wake wakubwa.
Na Michael Momburi MWINA Kaduguda amedai kuwa hakuna kiongozi yoyote wa timu hizo ambae anapenda kusikia mechi ya watani ya jadi. Katibu huyo mkuu wa kuchaguliwa wa Simba, alisema jijini Dar es Salaam kuwa licha ya kwamba viongozi hutamba hadharani lakini moyoni huumia sana. "Mechi inayokutanisha Simba na Yanga hakuna kiongozi yoyote wa hizo timu anayeipanda, ni mechi ngumu sana na yenye mambo mazito," alidokeza Kaduguda. "Kwanza gharama ni nyingi mno tofauti na watu wa kawaida wanavyofikiria, halafu kwa viongozi hatutulii, mpaka mkeo nyumbani anakuwa hana raha. "Kwa mfano mimi muda wangu wa kulala kwa wiki ambayo tunafanya maandalizi ya hiyo mechi siwezi kulala chini ya saa 6 usiku. "Hata nikilala lazima utasikia kiongozi fulani kakuamsha muda fulani kuashiria kwamba kuna mambo yakufanya au hata wazee, yaani ni mechi ngumu sana ambayo hakuna kiongozi wa timu yoyote kati ya hizo mbili anayeipenda." Mshambuliaji wa Yanga, Boniface Ambani alitamka hivikaribuni kwamba anashangazwa jinsi viongozi wa Yanga walivyokuwa wakijiandaa na mechi dhidi ya Simba tofauti na Ligi ya Mabingwa Afrika.

0 comments

Post a Comment