Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Nani kasema Ukoloni umeisha Africa? Au nani anabisha kuwa bado Waafrica ni Watumwa? Ukiweka Mzungu basi mtakuwa matajiri.....

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter Jacob Zuma atangaza baraza la mawaziri
Trevor Manuel, aliwahi kuwa waziri wa fedha wa Afrika Kusini.
Bw Manuel anasifika kwa kuimarisha vyema uchumi wa Afrika Kusini.
Rais mpya wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, amemtangaza Pravin Gordhan kuwa waziri mpya wa fedha wa nchi hiyo. Atapokea kiti kutoka kwa Trevor Manuel, ambaye sasa ametuliwa kusimamia mipango ya uchumi.

Bw Zuma ameahidi kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi, umasikini uliokithiri na uhalifu unaoongezeka, lakini akasisitiza kuwa hatawapendelea wafuasi wake.

Bw Gordhan alikuwa akifanya kazi katika idara ya kodi na amesifiwa kwa kuimarisha mapato ya serikali.

Baraza la Mawaziri
Makamu wa rais: Kgalema Motlanthe
Tume ya Mipango: Trevor Manuel
Usimamizi na Tathmini: Collins Chabane
Fedha: Pravin Gordhan
Sheria: Jeff Radebe
Ulinzi: Lindiwe Sisulu
Afya: Aaron Motsoaledi
Mambo ya Nje: Maite Nkoana-Mashabane
Makazi: Tokyo Sexwale

Akiwa mkuu wa kitengo cha taifa cha mipango, Bw Manuel sasa atakuwa na majukumu ya kupanga mikakati na kusimamia uratibu wa shughuli za idara za serikali.

Bw Manuel amesifiwa kwa kuongoza vyema uchumi wa Afrika Kusini kwa miaka 13, anaondoka wakati uchumi unayumba kote duniani.

Aaron Motsoaledi amepewa jukumu la kusimamia wizara nyeti ya Afya. Atakuwa na jukumu la kuongoza mapambano dhidi ya maradhi ya HIV na UKIMWI nchini humo.

Madaraka

Bw Zuma alichaguliwa na bunge kuwa rais baada ya chama cha African National Congress kushinda uchaguzi mkuu mwezi Aprili. Aliapishwa siku ya Jumamosi kuchukua hatamu ya kuongoza taifa la Afrika Kusini kama rais mpya.

Kiongozi huyo alikula kiapo mbele ya wageni waalikwa 5,000 na wafuasi wa ANC waliokusanyika kwenye majengo ya Muungano (Union Buildings) katika sherehe hizo mjini Pretoria.

Tags:

0 comments

Post a Comment