|
Wanasheria wa serikali Afrika Kusini wapinga kuachiwa Zuma |
Tuhuma hizo zilikataliwa na mwezi wa Septemba kutokana na sababu za kiufundi na kuibua mtikisiko wa kisiasa uliosababisha Rais Thabo Mbeki kujiuzulu.
Jaji aliyesikiliza kesi hiyo aliwashutumu waendesha mashtaka wa serikali kwa kuingilia kesi hiyo kwa sababu za kisiasa.
Bwana Zuma anapewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi mkuu utafanyika mwakani.
Kiongozi huyo wa ANC amefika mahakamani kusikiliza kesi yake. Ulinzi umeimarishwa sana nje ya mahakama kuu ya rufaa katika mji wa Bloemfontein.
Bwana Mbeki amekanusha tuhuma za kuingilia kisiasa kesi ya Zuma, lakini rufaa yake ikashindwa dhidi ya hukumu hiyo ya jaji mwezi uliopita.
Lakini anatazamiwa kuomba mahakama imruhusu awe sehemu ya kesi hiyo.
Anasema Bwana Mbeki haikuwa haki kwa Jaji Chris Nicholson tkupitisha hukumu kutokana na uamuzi wa serikali yake bila ya kumpa nafasi ya kujitetea.
0 comments