|
Kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai |
Hata hivyo, Bw Nelson Chamisa amesema maswala mengine bado hayajapatiwa suluhu kabla ya serikali ya muungano kuundwa.
Mabadiliko yaliyofikiwa nchini Afrika kusini yamemwandalia njia kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai kuwa waziri mkuu kama yalivyofafanua makubaliano ya mwezi Septemba.
Pande zinazopingana bado hazijakubaliana juu ya mgawanyo wa nafasi za baraza la mawaziri.
Rais Robert Mugabe ambaye pia ni kiongozi wa chama cha Zanu-PF na Bw Morgan Tsvangirai anaeongoza chama cha MDC walikubaliana kugawana madaraka ili kuokoa uchumi wa nchi hiyo, baada ya kufanyika uchaguzi wa kutatanisha.
0 comments