Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - HOJA ILIYOWASILISHWA KWA BUNGE LA WANAFUNZI WA TANZANIA.

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
HOJA ILIYOWASILISHWA KWA BUNGE LA WANAFUNZI WA TANZANIA.
Yah : HOJA YA KUTAKIWA KUJIUZURU KWA UONGOZI WA TSU NA BUNGE KUSHIKA MADARAKA KIKAMILIFU YA KIUTENDAJI KWA MASLAHI YA JUMUIA YETU.
Husika na kichwa habari , Kikao cha wanachama wa TSU (jumla ya wajumbe 10 na wawakilishi wa jinsia zote) toka sehemu mbalimbali wenye uchungu na muelekeo wa jumuia yetu tulianayo sasa, tulikutana tarehe 15.11.08 block 10 chumba 315. kuanzia saa mbili hadi saa tano usiku, kwa lengo kutathimini hali ya kijamii, kielimu , kiuchumi na kiungozi ndani ya jumuia yetu . Kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa (katiba), sisi kama wanachama wa jumuia yetu, na kwa kushirikiana na wajumbe wengine wenye mawazo ya busara na endelevu, tumeona ni vema kuleta hoja hii mbele ya bunge lako tukufu, na kuitishwa mara moja kwa kikao cha bunge ili kupitia mapendekezo ya wajumbe kwa manufaa na ustawi wa jamii yetu hapa chuoni. Kwa kunusuru hali ya mambo iliyopo(migomo na maandamano) itakayoendelea kwa muda usiojulikana(kama ilivyo ahidiwa na mw/kiti wa TSU),wajumbe wa kikao wamepitia mwenendo mzima wa utendaji wa viongozi wa TSU tangu washike madaraka 30.6.2008, na haswa hali ya sintofamu iliyoanza kujitokeza kuanzia Sept 2008 inayolenga jumuia yetu nzima hapa chuoni. Wajumbe wa kikao husika wamegundua ukeukwaji wa vipengere vya katiba unaofanywa na viongozi walioko madarakani , mfano :- kipengere cha sifa za kiongozi ; {5.2.1} ,{5.2.3}, {5.2.5}, {5.2.6} n.k. Wajumbe husika wa kikao, tumetathimini uongozi wa TSU chini ya Mw/kiti Kanyathare B.E. na kugundulika kuwa na makosa ya kiutendaji kama ifuatavyo:- 1).Baadhi yaViongozi wamekuwa mstari wa mbele kushinikiza migomo na kuvuruga amani hapa chuoni. 2). Baadhi ya viongozi wanatumia lugha za uzalilishaji(kinyume na katiba) na kutokuwa na heshima kwa wanafunzi na watendaji wa serikali. 3.) Uhusiano usio wa kuridhisha kati ya viongozi wa TSU na uongozi wa chuo. 4).Uhusiaono mbaya zaidi wa viongozi wa TSU na ubalozi wetu , kwa kujenga chuki katika jumuia yetu dhidi ya ubalozi bila kuwa na fact za kimaandishi na pasipo kufuata utaratibu za kiutendaji . 5). Baadhi ya viongozi kuchukua jukumu la kuwatishia amani, na hata kuwapiga (kwa kuwafuata chumba hadi chumba) wale ambao hawakushiriki /hawataki kujitokeza katika migomo inayohamasishwa na viongozi. 6). viongozi kutokukubali kukosolewa , na kushauriwa (kikatiba) kwa maslahi ya ustawi wa jamii yetu 7.)Viongozi kutokukubali /kutokuwa tayari kutumia njia za kidipromasia kama mchakato wa utendaji wa kinidhamu na utashi kwa maslahi ya jumuia nzima. Refer viongozi wafuatao walitamka wazi ndani ya mkutano mkuu sept 2008. “hawako tayari kutumia dipromasia katika kutatua matatizo” Kanyathare B.E(mw/kiti), Kwagirwa R.N( naibu katibu mkuu), Rusesa Ally M.(katibu michezo) na Pazi Husein (naibu katibu-michezo) 8).Baadhi ya viongozi (hasa waliotajwa) kukosa dira na muelekeo katika uadilifu ,utashi ,na nidhamu za kiungozi katika njia za kimantiki za kutatua matatizo yanayoikumba jamii yetu ,lengo lao ni kuisumbua jamii ya watanzania hapa chuoni. Mh.spika ,. kwa kuzingatia hoja hizo za msingi , na kunusuru kupoteza thamani ,umoja na mshikamano ndani ya jumuia yetu hapa chuon na kwa maslahi ya waliopo na watakao kuja, tunajenga hoja zifuatazo:- A) kutolewa mualiko rasmi toka kwa spika , kwa baadhi ya wanajumuia wenye busara na utashi kuhudhuria vikao vyote vya bunge kama wachangiaji mada, na kushauriana na waheshimiwa wabunge ili kupata muelekeo mzuri wa maamuzi ya kiutendaji ndani ya jumuia. B) Kwa kuzingatia ukeukwaji wa katiba, mahusiano yasiyo ya kuridhisha na chuo, mahusiano mabaya zaidi na ubalozi ambaye ndio mlezi wa jumuia ,na ishara za kuanza kugawanyika kimakundi ndani ya jumuia: ‘uongozi wa TSU hauna budi kujiuzuru” kwa kushindwa kuiongoza jamii yetu. C) Wanafunzi wafuatao:- Kanyathare B.E, Kwagirwa R.N, Lusesa Ali. M. na Pazi Husein. Kwa kipindi hiki “Wasijuhusishe” na shughuri zozote au kugombea uongozi wowote ndani ya jumuia yetu, na hawatakiwi kujibu hoja yoyote kwa mtu yeyote au kundi lolote la wanafunzi , mpaka pale watakapohitajika kufanya hivyo kwa ruhusa ya bunge lako tukufu. D) Spika wa bunge na Naibu wake ,wakishirikiana na wabunge kuteua watu toka katika jumuia na baadhi ya viongozi wa TSU wenye busara , nidhamu, uadilifu na utashi wa kiutendaji ambao wakishirikiana na Spika wa bunge Bw. SWILLA Livingston. (kama co-chairman of TSU), ili kurejesha uhusiano na utendaji wa jumuia katika nyanja zifuatazo.:- i)kurejesha mahusiano mazuri baina ya wanafunzi wa Tanzania na uongozi wa chuo na ubalozi. ii) kuendeleza Taratibu zote za kuwapokea wanafunzi wapya na kuhakikisha wanasajiriwa na chuo na kupatiwa makazi ya kudumu(hostel) hapa chuoni. iii) kuhakikisha wanafunzi wapya wananza kusoma masomo ya lugha(patfak) haraka ili kuepukana na adhabu ya kusoma kwa muda wa miaka miwili patfak badala ya moja kama kawaida kwa kuwa wamechelewa kuja urusi na wanazidi kuchelewa kuanza kozi hiyo. iv) kushughulikia matatizo ya pesa za wanafunzi 12 ambao hawajapata toka bodi ya mikopo na wanafunzi wa mwaka wa lugha 2008/2009 ambao wanaendelea kufika, kwa njia za kujenga hoja za kimsingi wakishirikiana na ubalozi wetu ili ufumbuzi upatikane mapema zaidi kutokana na ukata wa kimaisha walionao wenzetu. E) Spika wa Bunge( as acted co-chairman of TSU) unashauliwa utoe ujumbe kwa wanajumuia, kwa kupiga vita , kulaani na kukomeshwa mara moja vitendo vyote vinavyoendelea kuandaliwa na baadhi ya viongozi wakishirikiana na wanafunzi wachache- kwa kujenga chuki dhidi ya watendaji wa ubalozi, kuandaa maandamano dhidi ya ubalozi bila ya kuwa na hoja yakinifu,kukeuka sheria za serikali ya urusi, kuwahimiza wenzao kutoingia madarasani kinyume na taratibu za chuo. F) Spika wa bunge na kamati yako ya uteuzi, ukishirikiana na Uongozi wa chuo - unashauriwa uandae mkutano na wanafunzi wote wa 2008/2009 ili kuelezwa na kufafanuliwa taratibu na sheria za serikali ya urusi ,chuo,hostel na hali halisi ya maisha hapa urusi. G) Spika kutoa taarifa za kuondolewa madarakani viongozi husika na hatua za kinidhamu dhidi yao na sisi wanachama (tulioleta hoja hii) na wanafunzi wote tutahakikisha adhabu watakaopewa inatekelezeka kikamilifu chini ya maamuzi ya bunge lako tukufu H)Spika wa bunge unashauriwa kuandika barua kwa Mh. Barozi, ukimsihi asitishe hatua zozote za kiutendaji ambazo anataka kuzichukua dhidi ya wanafunzi Fulani au dhidi ya jumuia nzima wakishirikiana na uongozi wa chuo kutokana na wanafunzi wachache .Wakati ambao tunalitumia bunge lako kuleta Amani na masikilizano ndani ya jumuia. I) Spika unashauriwa uitaarifu jumuia nzima, kuwa- mwanafunzi yeyote ambaye hana dhamira za uanafunzi,na ameshindwa kusoma ni vema Andike barua wizarani kupitia ubalozi ,aombe kwa hiari yake kurudishwa nyumbani sio kusumbua jamii inayohitaji kupata elimu kwa manufaaa ya Taifa letu changa la jamhuri ya muungano wa Tanzania. Kwa kuzingatia vifungu mbalimbali vya katiba na kwa lengo la kuimarisha umoja wetu na wadogo zetu watakaokuja kusoma katika chuo hiki, na kwa kulinda heshima ya mtanzania hapa chuoni kama jumuia na kwa niaba ya wanafunzi wote(ambao ni zaidi ya 80%) ambao wameguswa na hali hii inayoendelea ambayo haitatusaidia katika kipind hiki kuimarisha bali inabomoa jamii yetu, ndio maana tumeleta hoja hii. Na kwa manufaa ya wanafunzi wenzetu,dada, kaka, na wadogo zetu ambao wanaendelea kuja kusoma hapa Lumumba kwa lengo na madhumuni ya kusaidia familia zetu, jamii zetu huko nyumbani na hasa zaidi kulitumikia Taifa Letu changa. Mh! Spika , Tunaomba kutoa hoja!
Tags:

4 comments

  1. Anonymous says:

    Mheshimiwa Spika naomba kuunga mkono hoja.

    Ila naomba ufafanuzi juu ya hili: "What do exists among T.S.U members between permanent friendship and permanent interest? If the later exists basi suala la uongozi litakuwa tatizo vizazi na vizazi daima na milele. Amen!

    Wenye macho wataona na wenye ufahamu watanielewa nazungumzia nini hapa.

    Mbarikiwe sana.

  2. Anonymous says:

    kwa ujumla viongozi mliopo madarakani acheni kutumia madaraka yenu mkidai haki au mkifikiri kwamba njia mnazozitumia ni sawa . tangu mmeingia madarakani ni matatizo tu ndio yanazidi wanafunzi wanaanza kuwa na uhusiano mbaya na chuo watanzania tunaonekana wakorofi , jamani tanzania ni nchi pekee iliyokuwa ikisifika kwa taaluma ya juu na heshima chuoni kwa kipindi cha muda mrefu tangu miaka ya 70. tafadhali rudisheni heshima ya nchi kwa kasi kama mlivyoishusha. Hatutaki sifa mbaya kaeni nazo hukohuko wengine wenu mlifukuzwa vyuo huko tanzania kwa sababu mnazozijua wenyewe sasa basi machafuko yenu ni kero kwetu sisi wana jumuiya. Msituletee sumu zenu, madaraka sio ya kungangania na subirini mtatolewa vivyo hivyo kama mlivyoshinikiza wenzenu watoke . Muda umefika tunataka mbadiliko. Tumieni busara

  3. Anonymous says:

    Naunga mkono hoja! Tumekuja kusoma sio kujifunza siasa. Viongozi jiachieni, tunataka mabadilko b4 januari! wendawazim wote(kwagirwa,boni wao,mkada na pazi) hamna pumzi jiachien, tulikuwa tunawaamini hamna lolote, Tunawato sasa, mtake msitake. ule mgomo wenu uko wapi sasa, tepeee! Mmewajaza chuki madogo sasa wamewageuka na hamna saport.! Mko hoi, presure zimepanda! Mnaweweseka, na bado,mpaka chupi ziwabane! Gwagirwa umebana mwisho umeachia! TSU INA WENYEWE hujui?

  4. Anonymous says:

    TSU ina wenyewe, na wenyewe ni mimi na wewe tunaosoma hapa Lumumba, period!

Post a Comment