Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Kamanda wa jeshi la Uingereza akiri kushinda vita na Taliban haiwezekani

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Kamanda wa majeshi ya Uingereza yaliyoko nchini Afghanistan amesema kuwa si rahisi kushinda vita dhidi ya kundi la wanamgambo wa Taliban.

Kamanda huyo Brigadier Mark Carleton-Smith amenukuliwa na Gazeti la Sunday Times la Uingereza akisema kuwa iwapo Taliban watakubali kuingia katika mazungumzo ya amani litakuwa jambo bora linalohitajika kumaliza vita nchini Afghanistan.

Lakini Waziri wa Ulinzi wa Afghanistan Abdul Rahim Wardak ameeleza kukatishwa tamaa na kauli ya kamanda huyo wa majeshi ya Uingereza akisema hayo ni mawazo yake binafsi.

Mjini Washington msemaji wa Ikulu ya Marekani Gordon Johndroe amesema kuwa matamshi ya kamanda huyo wa majeshi ya Uingereza, yanaashiria umuhimu kwa Marekani, NATO na jeshi la Afghanistan kushirikiana zaidi katika vita hivyo.

Marekani imepanga kuongeza kiasi cha wanajeshi elfu 8 ifikapo mwakani na kufanya idadi ya wanajeshi wake huko kufikia elfu 33.

Uingereza ina kiasi cha wanajeshi elfu 8 wengi wakiwa katika jimbo lenye ghasia la Hemland, ambako wamekuwa wakikabiliwa na mashambulizi kila mara kutoka kwa wanamgambo wa Taliban.

Kumekuwa na taarifa ya kwamba maafisa wa serikali ya Afghanistan na wale wa kundi la Taliban wamekuwa katika mazungumzo chini ya upatanishi wa mfalme wa Saudi Arabia.

Wiki iliyopita Rais Hamid Karzai wa Afghanistan alimuomba mfalme wa Saudi Arabia kusimamia mazungumzo ya amani na Taliban na kutoa wito kwa kiongozi wa kundi hilo Mullah Omar kurejea nchini humo ili kurejejsha amani.

Tags:

0 comments

Post a Comment