Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Moro yashuka daraja wakati Simba ikitwaa ubigwa. , Ngasa apiga la 14,

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
BAADA ya kukosa ubingwa mshambuliaji Mrisho Ngassa ameendeleza mbio zake za kuwania tunzo ya ufungaji bora kwa kufunga mabao mawili na kuisaidia Yanga kuionyesha Moro United njia ya kushuka daraja baada ya kuichabanga kwa mabao 3-0.

Mfungaji huyo bora wa Kombe la Chalenji 2010, Ngasa alifungua karamu ya mabao kwa Yanga dakika 5, ya mchezo alipounganisha kwa umakini krosi kutoka kwa Shamte Ally, kabla ya kupachika bao lake la 14 na la pili kwa Yanga dakika 31, akipokea pasi mkongwe Bonifance Ambani.

Ngasa ambaye kabla ya mchezo huo alikuwa nyuma kwa mabao mawili kwa Musa Hassan Mgosi aliyeiongoza Simba kutwaa ubingwa kwa kufunga mabao 14, huku Jumapili akishindwa kuziona nyavu dhidi ya Azam.

Ambani mfungaji bora wa msimu uliopita alifungia Yanga bao la tatu akimalizia krosi ya Shamte aliyekuwa mwiba mkali wa ngome ya Moro kutokana na kasi yake.

Moro ambao katika kipindi chote cha kwanza walikuwa wamekaa golini kwao wakijaribu kuzuia mashambulizi, lakini walishindwa kutokana na mipango thabiti ya vijana wa Mserbia Kostadic Papic.

Hivyo kumlazimisha kocha wa Moro kufanya mabadiliko kwenye safu yake ya ulinzi kwa kumtoa Said Omary na kumwingiza Thomas Ulimwengu aliyesaidia timu yake kwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa mabao 3-0.

Kipindi cha pili Yanga ilionekana kulidhika na ushindi wake kwa washambuliaji wake Ngasa, Abdi Kassim kupoteza nafasi nyingi za wazi za kufunga wakiwa wamebaki wao na kipa.
Kwa matokeo hayo Moro United imekuwa timu ya kwanza kushuka daraja msimu huu na sasa kibarua kimebaki kwa Toto African, Manyema na Prisons kupata timu nyingine mbili za kuunganao.

Kocha msaidizi wa Moro, kipa wa zamani wa Yanga, Juma Pondamali alikataa kuzungumza lolote baada ya filimbi ya mwisho, huku Papic amewasifu wachezaji wake kwa mchezo mzuri.

"Tumecheza vizuri katika dakika zote tatizo nililoliona kwa washambuliaji kukosa umakini kwenye umaliziaji nitalifanyia kazi kabla ya mechi yetu ijayo dhidi ya Simba."

Wakati huo huo: Doris Maliyaga anaripoti kuwa; Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea tena leo kwa kuwakutanisha maafande wa JKT Ruvu dhidi ya Manyema Rangers mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo unategemewa kuwa mgumu na wa aina yake kutokana na matokeo ya nyuma, JKT Ruvu iko kwenye nafasi ya nane na pointi 23 inazidiwa na Kagera Sugar ambao wana pointi sawa wakitofautiana mabao.

Manyema iko kwenye nafasi ya tisa na pointi 18, baada ya kuifunga Majimaji ya Songea iliyo kwenye nafasi ya tano magoli 2-1 wiki iliyopita, wanajua wakipoteza mchezo huo watakuwa wanasafisha njia yao ya kushuka daraja.

Kama JKT itapoteza leo itakuwa imejiweka katika mazingira mabaya kwa kuwa timu zilizo chini yake zinapointi 18 ambayo ni Manyema iliyo nafasi ya nne kutoka mwisho na wakati inayoshika mkia ina pointi 15 ambayo ni Moro United, Toto Africa 17, Prisons 17.
Tags:

0 comments

Post a Comment