Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden alifanya ziara nchini Israel kuhimiza msimamo wa Marekani kuhusu kuiunga mkono nchi kabla mazungumzo ya amani kati yao na wapalestina kuanzishwa upya.
Lakini kibao alichopigwa huenda kimechochea utawala wa Marekani kuchukua hatua. Washington haikutosheka tuu na kuelezea jinsi ilivyoghadhabishwa kulingana na msemaji wa ikulu ya whitehouse Phillip Crowley
Bw Crowley amesema Waziri wa mambo ya nje Bi Hilary Clinton amemfahamisha Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuwa wamechukizwa na hatua hiyo na kuwa wanahisi inahujumu mikakati ya kuleta amani Mashariki ya Kati.
Marekani imenuia kuishurutisha Israeli itamke kuwa ipo tayari kuzungumzia kuhusu suala la hatma ya mji wa Jerusalem mazungumzo ya amani yatakapo anza upya.
Lakini akilihutubia bunge Waziri Mkuu Netanyahu alionekana kutolegeza kamba kwenye msimamo wake.
Baadhi ya wadadisi siasa za mashariki ya kati, wanasema hatua ya Israel ilikuwa nzuri ilikuikumbusha Marekani kuhusu msimamo wake kuhusu amani Mashariki ya Kati.
0 comments