JERUSALEM
Waziri wa Ulinzi wa Israel Ehud Barak ametoa wito kwa Urusi kutoyauzia mataifa ya kiislam silaha kwani kwa kufanya hivyo kutatishia hali ya utengamano katika eneo la Mashariki ya Kati.
Waziri huyo wa Ulinzi wa Israel alisema hayo wakati alipokuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Bernard Kouchner mjini Jerusalem hapo jana.
Ehud Barak leo hii anatarajiwa kuanza ziara ya siku mbili nchini Urusi, ambapo agenda kuu ya ziara yake hiyo inategemewa kuwa ni mpango tata wa nuklia wa Iran.
Vyombo vya habari vya Israel vimearifu ya kwamba nchi hiyo haifurahishwi na mpango unaolezwa ya kwamba Urusi huenda ikaiuzia Iran makombora ya masafa marefu.
Mwezi uliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Tzipi Livni alielezea kusikitishwa na ripoti ya kwamba Urusi iko tayari kuiuzia silaha Syria nchi ambayo ni adui wa muda mrefu wa Israel.
0 comments