Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amewasili mjini Moscow

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amewasili mjini Moscow kwa mazungumzo na rais wa nchi hiyo Dmitry Medvedev juu ya mzozo wa Georgia.

Anajiunga na mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Javier Solana, na rais wa halmashauri ya Ulaya Jose Manuel Barroso.

Mkutano huo unakuja baada ya mzozo kati ya Urusi na Georgia kuhusiana na jimbo linalotaka kujitenga la Ossetia kusini. Rais Sarkozy anatarajiwa kuishurutisha Urusi kutekeleza kikamilifu mpango wa amani wa umoja wa Ulaya ambao rais Sarkozy alikuwa mpatanishi wiki nne zilizopita na kumaliza mapigano.

Mataifa ya magharibi yanaishutumu Urusi kwa kubakisha baadhi ya majeshi yake ndani ya Georgia wakati ilipaswa kuyaondoa hadi katika eneo la kabla ya mzozo.

Urusi inasema makubaliano ya kusitisha mapigano ya mwezi uliopita yanaipa nafasi ya kuweka majeshi yake katika eneo la amani.

Wakati huo huo shutuma za Georgia kuwa Urusi imefanya ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya Wageorgia katika jimbo linalotaka kujitenga la Ossetia ya kusini na Abkhazia yamefikishwa katika mahakama ya kimataifa leo Jumatatu.

More news | 08.09.2008 | 11:00 UTC

Tags:

0 comments

Post a Comment