Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - UTEUZI WA NAIBU GAVANA BENKI KUU YA TANZANIA

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Daktari Natu El-Maamry Mwamba kuwa Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania. Dkt. Mwamba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt Enos Bukuku, ambaye aliteuliwa kuwa Naibu Katibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwezi April, 2011. Uteuzi huu unaanza tarehe 13 Juni, 2011.


Kabla ya uteuzi huu, Dkt Natu El-Maamry Mwamba, alikuwa mhadhiri mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Uchumi.


Phillemon L. Luhanjo


Katibu Mkuu Kiongozi


Ikulu,


Dar Es Salaam

0 comments

Post a Comment