SERIKALI imesema imechoka kuburuzwa na masharti ya wahisani wanaosaidia bajeti na sasa inaangalia uwezekano wa kujitegemea katika bajeti zake kwa asilimia zote.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhani Khijjah, alisema hatua hiyo inalenga katika kuepuka misaada inayoweza kulitumikisha taifa.
Alisema hayo katika mkutano wa siku mbili wa kujadili uwajibikaji wa pamoja katika matumizi ya fedha za wahisani kwenye maendeleo, ulioandaliwa na wizara hiyo.
Khijjah alisema serikali inaangalia jinsi gani ya kujitegemea katika bajeti yake kwa kuwa haitaki wahisani wawe wanaiongoza kutokana na misaada yao wanayotoa.
Kwa sasa bajeti ya serikali inasaidiwa na nchi wahisani 14.
"Siyo tu wahisani wawe wanatoa masharti bali na wao tuwe tunawaelekeza. Wahisani kazi yao ni kusaidia tu na nchi ni kuongoza,"alisema.
Khijjah alisema serikali haitaki kuongozwa na wahisani bali serikali ndiyo iwe inawaongoza kwani misaada yao ni ya muda.
Kwa mujibu wa Khijja ili kuondokana na tatizo hilo, Tanzania sasa inapaswa kujipanga kuondokana na utegemezi wa misaada ya wahisani.
"Tunafanya mpango wa kuongeza mapato ya ndani ili kuimarisha uchumi wa nchi na tuweze kukopa katika masoko ya fedha kwa gharama nafuu,"alisema Khijjah.
Lakini akaeleza kuwa ili mpango huo ufanikiwe, kunahitajika jitihada za pamoja kutoka kwa mashirika yasiyo ya kiserikali, vyama vya siasa na sekta binafsi kwa ujumla.
Mbunge wa Bariadi Mashariki UDP, John Cheyo alisema kuwa tatizo lililopo ni kuwa wazungu hawaziamini nchi za kiafrika na ndio maana hawatoi fedha nyingi.
Cheyo ambaye ni mshiriki katika mkutano huo, alisema kuwa misaada inatumika zaidi kuziongoza nchi masikini na si kuzisaidia.

0 comments