Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Cheyo, Nape watupa kombora lao Dowans

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
MBUNGE wa Bariadi Mashariki, John Cheyo, amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kuandaa maelezo ya kuwasilisha bungeni yatakayoonyesha wapi amepata Sh94 bilioni za kuilipa kampuni ya Dowans.

Cheyo alisema hayo jana katika mahojiano maalumu na gazeti hili kwenye mkutano wa kujadili uwajibikaji wa pamoja katika matumizi ya fedha za wahisani, uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Alisema fedha hiyo haiwezi kulipwa kwa kuwa haiko kwenye bajeti ya Serikali iliyotengwa na Bunge mwaka jana na ili ilipwe lazima bunge liidhinishe.

"Sh94 bilioni zinatoka wapi? Nimechukizwa sana na hili. Wanasema walipe ina maana kama watalipa na sisi ndiyo tulipitisha bajeti inaonyesha kuwa bajeti hupitishwa kwenye makaratasi tu,"alisema Cheyo.

Cheyo alisema kuwa anashangaa kwa nini Serikali inaharakisha kuilipa Dowans badala ya kuangalia uwezekano wa kuepukana na deni hilo ambalo kimsingi ni mzigo kwa taifa.

Kwa mujibu wa Cheyo, pamoja na kuwa Serikali inaharakisha jambo hilo, lazima itoe taarifa kamili bungeni kueleza wapi itapata fedha hiyo na malipo hayo yatafanyikaje.

"Nimehuzunishwa sana na hilo kwa kuwa malipo hayo yanatokana na udhaifu mkubwa katika masuala ya mikataba unaofanywa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na wizara,"alisema Cheyo.

Kauli hiyo ya Cheyo ni mwendelezo wa wadau kupinga malipo hayo baada ya juzi Kambi ndogo ya Upinzani bungeni kuonya kuwa, kama Serikali ya CCM ikilipa fedha hizo, ijiandae kujiuzulu huku Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, akisema tatizo ni jambo hilo, kutopitia kwenye Baraza la Mawaziri.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Nape Mnauye alisema kwamba haamini yale aliyoskia  juu ya kuwalipa Dowans ni uamuzi wa Kamati Kuu ya CCM anayoifahamu.

"Siamini kama yale niliyosikia juu ya kuwalipa Dowans ni uamuzi wa Kamati Kuu ya CCM ninayoifahamu. Katika mazingira ambayo hukumu ile haijasajiliwa nchini, utata juu ya wamiliki na uhalali wa mikataba ya Richmond na baadaye Dowans,"alisema

Nape alisema kwamba chama chake , CCM hakiwezi kufanya maamuzi kama hayo wakati kuna asasi za kiraia zimefungua kesi kortini kupinga hatua ya Serikali kuwalipa Dowans. "Nina mashaka kama taarifa iliyotolewa na CCM ni ile iliyoamuliwa na Kamati Kuu," alisema Nape

Naye Mhadhiri Msaidizi wa Shule ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Onesmo Kyauke, ameitaka Serikali ilipe kwanza deni la mfanyabiashara mwenye asili ya Asia Devram  Valambhia na Watanzania wote wanaoidai.

Kyauke ambaye pia ni wakili wa kujitegemea anaungana na wasomi, wanasiasa na watu wa kada mbalimbali ambao wanalaani hatua hiyo ya Serikali kutaka kuilipa Dowans.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kyauke alisema haoni sababu ya Serikali kuwa na uharaka wa kuilipa Dowans wakati kuna Watanzania wengi wanaidai kwa kipindi kirefu na hawajalipwa.

Mwanasheria huyo alihoji kwa nini Serikali ikazanie kuilipa Dowans wakati kuna  hukumu za nyuma za Watanzania ambazo hadi sasa bado hazijalipwa.

Valambhia anaidai Serikali kiasi hicho cha pesa yakiwa ni malipo ya magari kadhaa kutoka nchini Chechslovakia aliyoiuzia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa miaka ya 1980
Tags:

0 comments

Post a Comment