Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Mnyika ajitolea mshahara wake

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, John  Mnyika, ametoa asilimia 40 ya mshahara wake kwa kipindi chote cha ubunge wake kuchangia mfuko wa elimu na kituo cha elimu kinachotarajia kuanzishwa jimboni humo.

Akizungumza kwenye kongomano la lililoandaliwa na Kamati ya Mafunzo ya Elimu ya Juu ya Chadema kutoka vyuo vikuu vya Jiji la Dar es Salaam, Mnyika alisema tayari ameanza kutekeleza ahadi hiyo.

Mnyika alisema ametoa asilimia 20 ya mshahara uliopita na kwamba, lengo ni kutunisha mfuko huo.
Kuhusu ujenzi wa kituo cha elimu, Mnyika aliahadi kutoa asilimia 20 ya posho ya ubunge kila mwezi hadi ujenzi utakapokamilika, mradi huo unalenga kuimarisha elimu kwa watu mbalimbali jimboni humo.

Alisema taratibu za kushughulikia kituo hicho zitaanza na ndani ya miezi mitatau na taarifa itatolewa kwa wananchi.
Mradi huo uliibuliwa jana kwenye kongamano hilo na wawasilisha mada ya elimu waliodai kitasaidi kukutanisha wasomi kutoka maeneo mbalimbali kujadili masuala ya elimu.

Kuhusu utekelezaji wa ahadi zake, Mnyika alisema Januari anatarajia kukutanisha wataalamu mbalimbali, watendaji wa serikali na wanaharakati kujadili kwa pamoja jinsi ya kutatua tatizo la maji.

Mnyika alisema hali hiyo imelenga kutumia wataalamu wa aina zote kuhakiisha utatuzi wa kudumu wa kero ya maji jimboni humo inapatikana.
Kongomano hilo liliwakutanisha wanafunzi na wanaharakati toka asasi mbalimbali ikiwamo ya Haki Ardhi, mada saba ziliwasilishwa na kujadiliwa. 


Tags:

0 comments

Post a Comment