Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Mshindi Miss Kigoma anyang'anywa taji

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter KAMATI iliyoratibu shindano la kumtafuta Miss Kigoma mwaka 2010 imetengua ushindi wa mshindi wa tatu, Husna Habibu, kwa madai kwamba, hakuwa na sifa za kushiriki mashindano hayo kwa kuwa ana mtoto.

Mratibu wa mashindano hayo, Jumanne Gange amesema, ushindi huo ulitenguliwa saa mbili baada ya kutangazwa matokeo.

Gange amesema, dakika chache kabla ya kutangazwa matokeo walipata taarifa kwamba mshiriki huyo ana mtoto na kwamba, matokeo yalipotangazwa kamati ilikutana kujadili jambo hilo na hatua za kuchukua.

Wapenzi wengi waliohudhuria shindano hilo waliondoka wakifahamu matokeo ya awali na hata habari zilipozagaa mjini wengi hawakukubaliana na uamuzi huo.

Kamati hiyo imemtangaza aliyekuwa mshindi wa nne,Leah Michael kuwa mshindi wa tatu hivyo amepata nafasi kuuwakilisha mkoa huo katika mashindano ya Kanda yatakayofanyika mjini Dodoma.

Sanjari na kuvuliwa taji, Husna amenyang'anywa zawadi ya mshindi wa tatu, ambayo ilikuwa ikijumuisha fedha taslimu Sh. 100,000.

Kamati ya Mashindabo hayo inashutumiwa na baadhi ya wapenzi wa fani hiyo kwa madai ilijua mapema suala hilo, lakini kutokana na kuwa na washiriki wachache walilifumbia macho na kuamini asingepata nafasi ya tatu.

Gange amekanusha madai hayo kwa kusema kuwa,kamati haikufahamu kuwa Husna ana mtoto. Katika shindano hilo, Sabrina Ezekia, alitwaa taji la Miss Kigoma 2010,Yasinta Apolinary, alishika nafasi ya pili.
Tags:

0 comments

Post a Comment