Wataalamu huko Marekani kwa mara ya kwanza wamefanikiwa kuunda seli hai kwa kutumia asidi nasaba, DNA iliyounganishwa na vitu mbalimbali.
Wataalamu hao waliunda programu ya vinasaba na kuvipandikiza ndani ya seli pokezi.
Matokeo yake yakazaa vijiumbe maradhi vinavyofuata nyenzo za ileile DNA iliyounganishwa.
Ufanisi huu uliochapishwa katika jarida maarufu 'science', umeshangiliwa na ulimwengu wa sayansi kama hatua kubwa, ingawa wakosoaji wanasema viumbe sanisia vinaweza kusababisha madhara yasiyoelezeka.
Wengine wanasema kuwa manufaa ya teknolojia hii yametiwa chumvi.
Lakini wataalamu wana nia ya kuunda seli za bakteria hiyo ambayo itasaidia katika utengenezaji wa dawa na mafuta halikadhalika kumeza gesi zinazochafua mazingira.
Kundi hilo la wataalamu lililongozwa na Dr Craig Venter kutoka chuo cha J.Craig Venter huko Maryland na Carlifornia nchini Marekani.
Kabla ya hapo yeye na wenzake waliunda bakteria kwa kuchanganya zaidi ya kitu kimoja na baadaye kuoanisha mfumo waliotumia mwanzoni.
Sasa wametumia njia hiyo hiyo kwa kuunganisha bakteria ya awali na kuunda seli yenye chembechembe ambayo ina uhai na uwezo wa kujenga ramani ya kiumbe.
Dr Venter alifananisha mafanikio haya na ujenzi wa mtambo mpya wa programu ya kujengea seli na kuongezea kuwa mtambo huu unapoanza kazi yake moja kwa moja huanza kuzalisha nakili za chembechembe za ramani.
Dr Venter alisema, hii ni mara ya kwanza kwa programu ya DNA kuweza kumiliki seli, na nadhani ni fursa kubwa katika mabadiliko ya sayansi ya viwanda.
Tayari Dr Venter na wenzake wanashirikiana na makampuni ya dawa na mafuta kuunda na kujenga kromosomu za bakteria ambazo zitaweza kutengeneza mafuta yenye manufaa pamoja na dawa mpya.
Hata hivyo wakosoaji wamejitokeza kwa kusema kuwa manufaa ya uvumbuzi huu yametiwa chumvi mno.
Dr Helen Wallace wa shirika la Greenwatch linalosimamia maendeleo ya teknolojia ya maumbile nchini Uingereza, ameiambia BBC kuwa bakteria iliyoundwa kwa mchanganyiko wa vitu vingi inaweza kuwa na hatari.
Unapoweka viumbe wapya katika mazingira unaweza kusababisha janga.
Kwa kuweka bakteria hawa wapya hewani ili kumeza uchafu kutoka viwandani, ukweli ni kwamba unasababisha uchafu zaidi. Hatuelewi ni jinsi gani vijidudu hivi vitaishi katika mazingira.
0 comments