Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Tucta sasa kumburuta Kapuya mahakamani

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania,(Tucta)limeandaa notisi ya kumfikisha mahakamani, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Profesa Juma Kapuya na serikali yake, kwa madai ya kutangaza mishahara ya sekta binafsi bila kufuata taratibu za kisheria.

Hatua hiyo imekuja baada ya Tucta kudai kuwa, Waziri Kapuya ametangaza mishahara ya sekta binafsi, ambayo ina mapungufu katika baadhi ya vipengele.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholaus Mgaya, alisema uamuzi wa kumfikiosha mahakamani waziri huyo, umetoikana na kikao cha Bodi ya Tucta.

Alisema notisi kuhusu mpango huo itatolewa kabla ya Profesa Kapuya, kutangaza makubaliano ya kikao cha utatu ambacho kwa mujibu wa sheria, waziri anapaswa kuyatangaza ndani ya siku 21.

Alisema muda huo utamalizika Mei 29 mwaka huu.

“Kikao cha bodi kilichofanyika jana (juzi), kilifikia maamuzi ya kumshtaki waziri Kapuya kwenye mahakama ya kazi, kwa kosa la kutangaza mishahara bila ya kufuata taratibu za kisheria," alisema Mgaya.


Alisema kimsingi, serikali imewadanganya wafanyakazi wa sekta binafsi kwa kutangaza mishahara yenye mapungufu makubwa.
Hivi karibuni, serikali kupitia Waziri Kapuya, ilitangaza nyongeza ya mishahara ya sekta binafsi kwa ongezeko la asilimia mia moja.

Wakati huo huo,Mgaya amekanusha taarifa iliyotolewa jana na wananchi wasiofahamika kuwa ana mpango wa kuwania ubunge katika Jimbo la Muheza kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema).


Alisema watu hao wanataka kumchafulia jina lake.

Mgaya alisema kuwa, kutolewa kwa vipeperushi hiyo ni ishara ya kuwepo kwa maadui wanaotaka kumchafua hasa kwa ajili ya msimamo wake wa kutetea wafanyakazi.
"Mimi ni mwanachama wa Chama Chama Mapinduzi (CCM) Tawi la Mchafukoge, ninalipa kadi yangu ya uwanachama kila mwaka na natambulika kisheria na taratibu. Maadui zangu wasiingize mgogoro wa wafanyakazi na serikali kuwa wa kwangu,"aliongeza.
mwisho
Tags:

0 comments

Post a Comment