Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Meya wa Jiji la Mwanza Kizimbani kwa mauaji

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter MAMIA ya wakazi wa jiji la Mwanza jana walifurika kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa kushuhudia meya wa jiji lao, Leonard Bandiho Bihondo akipandishwa kizimbani kwa kosa la mauaji.

Meya huyo, ambaye alikamatwa juzi kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza mara baada ya kuwasili akitokea Dar es salaam, alifikishwa mahakamani hapo pamoja na watuhumiwa wengine watatu wanaoshtakiwa kwa kosa la kumuua katibu wa CCM wa Kata ya Isamilo, Bahati Stephano, 50.


Shauku ya watu kushuhudia tukio hilo la aina yake iliisha kwa baadhi kuambulia kufuatilia kesi hiyo madirishani kutokana na chumba cha mahakama kuwa kidogo.

Bihondo, 64, hakuonekana kuwa na wasiwasi na alitulia kwenye kiti mahakamani hapo huku watuhumiwa wenzake watatu wakihangaika kuficha nyuso zao hasa wakati wapiga picha walipokuwa wakihangaika kuchukua kumbukumbu nzuri ya tukio hilo.


Bihondo alifikishwa Mahakamani hapo na kusomewa mashataka hayo majira ya saa 8.30 akiwa na watuhumiwa wenzake, Jumanne Oscar, ambaye alikamatwa siku ya tukio, Baltazal Shushi na Abdul Hausi kwenye Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa Mkoa.


Akisoma maelezo ya mashataka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Augenia Lujwahuka, wakili wa serikali, Stephen Makwega alidai kuwa mauaji hayo yalifanyika Mei 14 majira ya saa 6.30 kwenye Mtaa wa Isamilo.
Wakili Makwega, ambaye anashirikiana na mawakili wengine wa serikali katika kesi hiyo ambao ni Zakaria Makwaya na Donasan Mwita, alidai zaidi kuwa kuwa watuhumiwa hao walifanya mauaji hayo kwa kukusudia.
Wakili huyo aliendelea kuiambia mahakama kuwa uchunguzi juu ya kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imefikishwa hapo kwa ajili ya kusomwa.


Katika kesi hiyo watuhumiwa hao wanne hawakutakiwa kujibu chochote juu ya shtaka linalowakabili kwa kuwa kesi inayowakabili ni kesi ya mauaji.


Akizungumza mahakamani hapo Hakimu Lujwahuka alisema mbali na kutotakiwa kujibu chochote, kesi hiyo haina dhamana hivyo watuhumiwa wote kwa pamoja walipelekwa mahabusu ya Butimba hadi Juni 4 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Tags:

0 comments

Post a Comment