IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
OFISI ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka wazi, inamtambua aliyekuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Fred Mpendazoe kuwa bado ni mbunge wa jimbo la Kishapu kupitia Chama hicho hadi hapo itakapopata taarifa rasmi kutoka CCM.
Mpendazoe ni mmoja wa wabunge machachari wa Chama Cha Mapinduzi ambao walipachikwa jina la makamanda wa ufisadi, kutokana na msimamo wao mkali dhidi ya wanaotuhumiwa kwa kutafuna fedha za umma au kutumia madaraka yao vibaya.
Mbunge huyo alitangaza kukukiacha chama chake na kijiunga kwenye Chama Cha Jamii (CCJ) Machi 30 mwaka huu na kusisitiza kuwa CCM sio mama yake, hivyo hatajilaumu kukihama, kwa sababu alikuwa anaishi kwa matumaini muda wote ndani ya chama hicho.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel alisema, “Ofisi ya bunge bado inamtambua Mpendazoe kuwa ni mbunge halali wa jimbo la Kishapu kwa sababu haijapata taarifa yoyote rasmi, kutoka kwake au chama chake cha awali.â€
“Kama Mpendazoe angekuja bungeni leo angekalia kiti chake kwa sababu hatuna taarifa yoyote ya maandishi ya kujiuzulu kwake,†alisema Joel.
Joel alisema Ofisi ya Bunge inatakiwa kuwa na barua rasmi ya maandishi ya kuthibitisha kwamba Mpendazoe amejiuzulu nafasi ya ubunge au amekihama chake.
Alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza wazi taratibu na sababu za kuacha ubunge wa Bunge la Jamhuri.
“Sababu ya kwanza ni kwa mbunge mwenyewe kujinasua katika chama chake na kupata vithibitisho vyote, kuugua kwa muda mrefu na madaktari wakathibitisha kuwa hawezi tena kuwahudumia wananchi,†alisema Joel.
“Mwisho ni kwa mwanachama kufanya vitendo vichafu na chama kikakunyang’anya uanachama,†alisema Joel.
Alisema Ofisi yake haiwezi kukurupuka kwa vile kuna mivutano baina ya Mpendazoe na Chama chake, jambo linaloisababisha ofisi yake kusimamia taarifa rasmi itakayotumwa aidha kutoka chama chake cha awali au yeye mwenyewe binafsi.
Alisema kulingana na taratibu na sheria za bunge, Mpendazoe bado anatambuliwa na ofisi ya bunge kuwa ni mbunge wa Jimbo la Kishapu.
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu jana, Mpendazoe alisema, “Mkurugenzi amejibu vizuri, ni kweli mimi bado ni mbunge, ila nilichofanya ni kutangaza kwa vyombo vya habari kujivua uanachama wa CCM.â€
“Ubunge wangu utakoma pale nitakapowasilisha taarifa ya maandishi kwa katibu wa bunge, nakusudia kufanya hivyo siku yoyote kuanzia sasa. Nina mambo yangu binafsi yakikamilika nitakwenda,†alisema.
“Siku ile niliyokutana na waandishi Machi 30, sikupata muda wa kwenda ofisi za bunge kupeleka taarifa yoyote, lakini kikatiba natakiwa niwasilishe taarifa kwa katibu wa bunge,†alisisitiza Mpendazoe.
“Nitakwenda kwa katibu wa bunge, lakini sikwambii lini hiyo ni taratibu zangu, mimi sio rais wala waziri mkuu. Lakini kikatiba na kisheria natakiwa niwasilishe taarifa ya maandishi katika ofisi ya bunge,†aliongeza Mpendazoe.
Alipoulizwa iwapo ataingia bungeni katika mkutano huu wa 19, Mpendazoe alisema hayo ni mambo yake ya faragha (private).
“Unataka nikuambie naenda bungeni halafu kesho muandike Mpendazoe aingia bungeni, mbona mlikuwa hamuniulizi kabla sijahama CCM, mimi ni mtu mdogo bwana sipaswi kutangaza safari zangu,†alisema Mpendazoe.
Alipoulizwa kwa sasa yuko katika mji gani wa Tanzani, Mpendazoe alikataa kuweka wazi na kujibu tu kwa ufupi.
“Nipo Tanzania……nipo Tanzania bara lakini kukusaidia zaidi ndugu mwandishi.â€
Kwa upande wake Katibu wa Kamati Kuu Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chilgati alisema suala hilo haliwahusu wao kwa kuwa, Mpendazoe aliwambia kwa heri na wao wakamwambia asante.
“Hilo ni suala lake binafsi na mamlaka ya bunge, sisi hatujamfukuza ila yeye ndiye alituaga na sisi tukamwambia asante, hatuna ugomvi na wewe,†alisema Chiligati.
“Kama tungemfukuza uanachama sisi ndio tungelazimika kuiandikia ofisi ya bunge kuwa huyu si mwanachama wetu tena, lakini kwa vile yeye mwenyewe ndiye amehama chama, suala hilo ni la kwake na mamlaka ya bunge watajua namna ya kulimaliza,†aliongeza Chiligati.
You Are Here: Home - - Ofisi ya Bunge: Mpendazoe bado ni mbunge wa Kishapu
0 comments