UN yajitenga na kashfa ya silaha ya Tanzania |
UMOJA wa Mataifa (UN) umekana taarifa ambayo iliyotolewa hivi karibuni ikieleza kwamba umoja huo umebaini kwamba Tanzania inajihusisha na biashara ya silaha nchini Congo ambako kikundi cha waasi kinapambana na serikali. Tayari serikali ya Tanzania imeshakanusha kuhusika kwenye biashara hiyo na kuitaka UN kuiomba radhi, ikidai utafiti huo ni kuipaka matope nchi ambayo imekuwa mstari wa mbele kuchochea amani barani Afrika. Katika taarifa ambayo UN iliisambaza kwa vyombo vya habari jana, umoja huo umekiri kwamba kikundi kilichotoa taarifa hiyo kinafanya kazi chini ya Baraza la Usalama lakini hakina mamlaka ya kutoa taarifa kwa niaba ya UN. UN imeeleza kwamba bado haijakabidhiwa taarifa ya kikundi hicho huru katika kuchunguza mambo nchini DRC, matokeo ya uchunguzi wao haupaswi kuchukuliwa kama mtazamo wa umoja huo. Taarifa hiyo iliyotolewa na ofisi za UN hapa nchini inasema: "Ripoti hiyo ilitolewa na kundi la wataalamu nchini DRC. Kundi hili liliundwa na Baraza la Usalama mwaka 2004 katika kuunga mkono makubaliano ya kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. "Kundi hili linanasimamia utekelezaji wa makubaliano ya kusalimisha silaha na kufuatilia vikundi vya nje vinavyochochea vita kwa kufadhili waasi silaha na fedha." Katika hatua iliyofikiwa na kundi hilo, UN inaeleza kwamba lawama hazipaswi kutupwa kwao bali kwa jopo hilo la wataalamu pamoja na uongozi wao nchini DRC. Jumapili iliyopita Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, taarifa hiyo ni ya uongo, hivyo Tanzania inastahili kuombwa radhi na wote wanaohusika kuiandaa ripoti hiyo. Waziri Membe alisema ni jambo lisiloingia akilini kuwa nchi kama Tanzania iliyofanya mambo mengi na kujitolea mhanga kwa kila hali kuleta amani na kujenga usalama katika eneo la kanda ya maziwa makuu, inaweza kushutumiwa kwa kutoa silaha kwa waasi wa Congo. |
You Are Here: Home - - Tanzania na Kashfa ya Kuuza silaha kwa waasi wa Congo
IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
0 comments