Hotuba ya rais wa Iran yazua hisia kali
Rais wa Marekani, Barrack Obama ameyakashifu matamshi ya rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad kwa baraza kuu la Umoja wa Mataifa na kuyataja kama matusi na ya kuudhi.
Rais Ahmedinejad aliliambia mkutano wa baraza hilo kuwa Marekani ilihusika yenyewe katika mashambulio ya kigaidi ya Septemba Kumi na Moja.
Katika Mahojiano na BBC, Rais Obama amesema matamshi hayo ni tofauti kabisa na maoni ya raia wa Iran kuhusu mashambulio hayo.
Lakini katika kikao na waandishi wa Habari jijini New York, Ahmedinajad alitetea matamshi yake na kutoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuanzisha uchunguzi kamili kuhusu mashambulio hayo ya Septemba 11 ambayo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu alfu tatu.
0 comments