Ahmadinejad azua tafrani katika mkutano wa UN
Zaidi ya wajumbe thelathini wakiongozwa na Marekani walitoka nje kwa hasira katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa hotuba ya rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad.
Waliondoka baada ya rais Ahmadinejad kuelezea kwamba Marekani yenyewe huenda ilihusika kupanga mashambulio ya Septemba 11, 2001, ili kuimarisha mashambulizi yake mashariki ya kati na kuilinda Israeli.
Marekani imeelezea kauli hiyo kama isiyovumika.
Akizungumza kuhusu mpango wa Nuklia wa serikali yake rais huyo wa Iran alikosoa vikwazo vya kimataifa dhidi ya nchi yake na kuelezea nishati ya nuklia kama zawadi kubwa.
0 comments