Hizi zinasemekana ni kauli za waziri Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba
Akizungumza kwa kujiamini na ujasiri, Simba alimtuhumu mama Kilango kuwa kelele zote anazozitoa kuwashambulia baadhi ya wabunge na watendaji wa serikali kwamba ni mafisadi, zilitokana na nongwa ya kukosa “Ufesti Ledi’ (kuwa mke wa rais).
Mbali na Mzee Malecela na mkewe, Waziri Simba pia alimgeukia Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi akimtuhumu kuwa anaendesha vyombo vya habari vinavyoichafua CCM na serikali yake kwa maslahi binafsi.
Pia alimshambulia Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, akiwatuhumu kuwa ni watu wenye njaa na kwamba wanalipwa fedha za kufanya kazi ya kupambana na ufisadi.
Waziri Simba alisema hata tuhuma dhidi ya Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, zimetokana na chuki binafsi.
Alisema uchunguzi wa kashfa ya rada ulishamalizika na Chenge akasafishwa na kuongeza kwamba, hata uchunguzi wa Richmond ulibaini kwamba hakukuwa na rushwa.
0 comments