Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Babu Seya kutumbuiza leo Dar

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

MWANAMUZIKI anayetumikia kifungo cha maisha katika gereza la Ukonga Dar es Salaam Nguza Viking 'Babu Seya' leo anatarajia kutumbuiza wafungwa wenzake katika gereza hilo. Akizungumza Dar es Saalam jana, Kamisha Mkuu wa Magereza. Augustino Nanyaro, alisema Babu Seya atatumbukiza kwa kuimba nyimbo zake mbalimbali kupitia bonanza maalumu ambalo limeandaliwa kwa ajili ya wafungwa wa gereza la Ukonga na kuwa litaanza saa tatu asubuhi hadi saa 8 mchana katika viwanja vya Magereza Ukonga na kwamba wakati wanaandaa bonanza hilo walikaa na Babu Seya na wafungwa wengine ili kupata ridhaa yao kama wapo tayari kushiriki. "Kesho (leo) Babu Seya na watoto wake wamekubali kuimba live katika bonanza maalumu ambalo limeandaliwa na kampuni ya magazeti ya Global Publishers and General Enterprises kwa kushirikiana na magereza na wadau wengine. Kwa bahati nzuri amekubali kuimba kwani angekataa tusingemlazimisha,"alisema Nanyaro. Alisema licha ya Babu Seya kutoa burudani pia wafungwa wengine wenye vipaji vyao nao wataonesha umahiri wao katika bonanza hilo katika michezo mbalimbali, ambapo pia wafungwa hao watashindana katika michezo ya mpira wa miguu, mpira wa wavu, riadha, kukimbia kwa gunia, kukimbia kwa kung'ata kijiko chenye yai la kuku, kucheza bao, kucheza dama, kwaya na muziki na kutakuwa na zawadi anuai. Pia alisema vifaa ambavyo wanamuziki watakaotumbuiza katika bonanza hilo watatumia vimetolewa na Kampuni ya African Stars Entertaiment inayomiliki bendi ya Twanga Pepeta. Kuhusu msanii Khalid Mohamed 'TID' kama anaweza kuwa miongoni mwa wafungwa watakaotoa burdani, alisema hawezi kwani yeye yupo Segerea. Naye Zahoro Mlanzi anaripoti kuwa katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Mratibu wa bonzani hilo Isaac Kijoti kutoka Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises iliyoandaa bonanza hilo, alisema wameamua kutoa fursa hiyo kwa wafungwa, ili kuwapa moyo na kutoa dhana ya wao kutengwa na jamii, kwani wana haki kama watu wengine.

Tags:

0 comments

Post a Comment