Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - Urusi yamuunga mkono Rais Assad wa Syria

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Urusi imemuunga mkono Rais Bashar al-Assad wa Syria anaeshinikizwa na jumuiya ya kimataifa. Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov amesema, kujiuzlu kwa Assad kutahatarisha majadiliano, kati ya serikali ya Syria na wapinzani wake, ambayo yamependekezwa na Umoja wa Nchi za Kiarabu. Lavrov alitamka hayo baada ya kukutana na Mkuu wa sera za nchi za nje wa Umoja wa Ulaya, Bibi Catherine Ashton mjini Moscow.


Nae Bibi Ashton kwa upande wake ametoa mwito kwa serikali ya Syria na makundi ya upinzani kusitisha machafuko.


Urusi, kama China, ilitumia kura yake ya turufu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kulipinga azimio la kuilaani serikali ya Assad kwa kutumia mabavu dhidi ya waandamanaji. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu 3,500 wameuawa nchini Syria, katika maandamano ya kumpinga Assad.

0 comments

Post a Comment