Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KISIASA , HABARI ZA LEO - Nape kizimbani Arusha leo kesi ya Lema

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
KESI ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), inatarajiwa kuendelea leo kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kupanda kizimbani kufafanua kauli yake kuwa chama chake kinajiandaa kulitwaa jimbo hilo kwenye uchaguzi mdogo.


Nnauye anadaiwa kutoa kauli kwamba wana uhakika wa ushindi wa Lema unaopingwa na wapiga kura watatu, wote wanachama wa CCM, utatenguliwa na mahakama na hivyo, kuwataka vijana wa chama hicho kujiandaa kwa uchaguzi mdogo utakaoitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).


Maneno hayo yanadaiwa kutamkwa na kukaririwa na Gazeti la Nipashe toleo la Oktoba 9, mwaka huu, ambalo pamoja na Nnauye, Jaji Aloyce Mjuluzi anayesikiliza shauri hilo pia alimwamuru mhariri wa gazeti hilo kufika mahakamani leo kuthibitisha iwapo kweli maneno yaliyoandikwa yalitamkwa
na kiongozi huyo wa CCM.


Uamuzi wa Jaji kuwaamuru Nnauye na mhariri wa gazeti hilo kufika mahakamani ulitokana na hoja ya Wakili wa utetezi, Method Kimomogoro aliyeomba kesi hiyo isikilizwe na majaji watatu au watano kutokana na mteja wake kuhisi kuwa hatatendewa haki kwa sababu tayari CCM kimetamba kunyakua jimbo hilo kwenye uchaguzi mdogo hata kabla ya kesi kusikilizwa.


Kimomogoro alihoji kwa nini CCM iliyofungua kesi 14 za kupinga uchaguzi kati ya mashauri 44 ya uchaguzi yaliyofunguliwa na vyama vingine nchini kote, watangaze kujiandaa kunyakua Jimbo la Arusha iwapo hawajahakikishiwa ushindi mahakamani?


Wapiga kura watatu wanachama na wafuasi wa CCM,


wanaoiomba mahakama itengue ushindi wa Lema kwa madai kuwa alitoa maneno ya kashfa dhidi ya aliyekuwa mgombea wa chama hicho, Dk Batilda Burian wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita ni Mussa Mkanga,


Agnes Mollel na Happy Kivuyo ambao wanawakilishwa na Mawakili, Alute Mughwai na Modest Akida.
Katika kuhakikisha haki inatendeka, wakili huyo wa Lema alipomuomba Jaji Mkuu, Othman Chande kuteua majaji watatu au zaidi kusikiliza shauri hilo.Hoja hiyo ilimfanya Jaji Mjuluzi kumhoji wakili huyo iwapo kauli yake ina lenga kumwomba ajitoe kusikiliza shauri hilo linalovuta umati wa watu kila inaposikilizwa.


Hata hivyo, Wakili Kimomogoro alisema kilichomsukuma kufikia hatua hiyo ni mwenendo wa kesi hiyo na kwamba endapo wangekuwapo majaji zaidi ya wawili, anaamini kwamba haki ingetendeka pasi na kutiliwa shaka.Umati wa watu umekuwa ukifurika mahakamani hapo kila kesi hiyo inapotajwa kiasi cha wengine kulazimika kubaki nje kutokana na ufinyu wa chumba cha mahakama.


Hata hivyo, habari njema kwa wale watakaokosa fursa ya kuingia ndani ya chumba kitakachotumika kuendeshea kesi hiyo ni kwamba watapata fursa ya kusikiliza mwenendo wake kupitia vipaza sauti ambavyo Jaji Mjuluzi aliagiza vifungwe.

0 comments

Post a Comment