Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - Muswada tata wapitishwa Afrika Kusini

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Bunge la Afrika Kusini limepitisha kwa kura nyingi muswada wa sheria tata kuhusu kulinda siri za serikali ambao umesababisha maandamano katika miji kadhaa nchini humo.
Wapinzani wa muswada huo wanasema sheria hiyo mpya inayopendekezwa inatishia usalama wa kujieleza na inakiuka katiba.
Askofu Mkuu Desmond Tutu ameielezea sheria hiyo kuwa haifai na ni matusi kwa wananchi wa Afrika Kusini.
Hata hivyo chama tawala cha African National Congress, ANC, kimesisitiza kuwa sheria hiyo inahitajika kulinda usalama wa taifa.
Muswada huo bado unahitaji kupitishwa na baraza la juu la bunge na Rais Jacob Zuma ili kuwa sheria.

0 comments

Post a Comment