Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - Merkel ashikilia kuubadili mkataba wa Umoja wa Ulaya

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Licha ya upinzani mkubwa kutoka Umoja wa Ulaya, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, anashikilia kuurekebisha Mkataba wa Umoja wa Ulaya, ili kuweza kuudhibiti mzozo wa madeni katika eneo la euro.


Kansela Merkel anazitaka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya, kukubali kuwa na viwango vya kukopa vinavyopaswa kuheshimiwa, kuziruhusu taasisi za umoja huo, kuingilia kati bajeti za taifa kwa kiwango fulani. Lengo ni kuwa na usimamizi bora wa kanuni za kusaidia kuleta utulivu wa sarafu ya euro.


Merkel amesema, nchi zinazokwenda kinyume na kanuni za mkataba wa Umoja wa Ulaya na kuhatarisha utulivu, zichukuliwe hatua.


Benki Kuu ya Ulaya isitumiwe kama chombo cha mwisho cha kusaidia katika mzozo wa madeni. Amesema, wanasiasa wanakosea kama wanaamini kuwa benki hiyo inaweza kusuluhisha tatizo la sarafu ya Euro iliyodhoofika.


Leo Kansela Merkel anakutana na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron mjini Berlin, kujadili hatua za kuchukuliwa kuhusiana na mzozo wa fedha.

0 comments

Post a Comment