Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - Libya yaishukuru Sudan

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Mkuu wa serikali ya mpito ya Libya, Mustafa Abdel Jalil, ameishukuru Sudan kwa msaada wake wakati wa kuiondoa serikali ya Kanali Muammar Gaddafi.


Akizungumza mjini Khartoum, Bwana Jalil alisema kuwa Sudan iliipelekea Libya silaha na risasi kwa kupitia Misri.
Serikali ya Sudan Kaskazini inapapambana na wapiganaji karibu na mpaka wake na Sudan Kusini, na katika jimbo la Darfur.
Waandishi wa habari wanasema kuanguka kwa utawala wa Kanali Gaddafi, kutaisaidia serikali ya Sudan kwa kuwanyima wapiganaji wa Darfur hifadhi.
Mustafa Abdel Jalil atafanya mazungumzo na wakuu kadha wa Sudan katika ziara yake ya siku mbili.

0 comments

Post a Comment