Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Kampuni ya Serena yanunua Mövenpick

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Kampuni inayojishughulisha na Huduma za Hoteli na Utalii Afrika Mashariki (Tourism Promotion Services (TPS) ambayo pia inamiliki hoteli za Serena imenunua hoteli ya Mövenpick Royal Palm ya jijni Dar es Salaam.


Kutokana na kununuliwa hoteli hiyo na TPS sasa itabadilishwa jina na kuwa Dar es salaam Serena Hotel kuanzia mwanzoni mwa mwezi ujao. Mövenpick Royal Palm Hotel ni hoteli yenye vyumba 230 na hadhi ya nyota tano.


TPS (D) Limited ndiyo kampuni ya ununuzi inayomilikiwa na Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED), TPS Eastern Africa Limited (TPSEAL), PDM (Holdings) Limited, PROPARCO and NORFUND .


Mkurugenzi Mtendaji wa TPSEAL, Mahmud Jan Mohamed katika taarifa yake kwa vyombo vya habari alisema kufunguliwa kwa hoteli za Serena jijini Dar es Salaa ni utekelezaji wa mpango wa muda mrefu wa kufungua hoteli katika miji mikuu Afrika Mashariki, yaani “City Hotel Circuit”


Alisema kutokana na kuwapo kwa hoteli tanzu za Serena, hoteli hii itafaidika na mtandao ulioenea Tanzania, Zanzibar, Kenya, Msumbiji, Rwanda na Uganda.


“ Lengo letu ni kupanua wigo wetu nchini na maeneo mengine. Hotel za Serena zinalenga kufikisha huduma bora kwa wateja wake, kutoa fursa za kazi za kuvutia kwa wafanyakazi wake,” alisema


Kwa sasa hoteli za Serena zina waajiriwa 3,400 kwa Afrika Mashariki.Jan Mohamed alisema Serena Hotels imepanuka kutoka vituo vinne mwanzoni mwa miaka ya 1970 hadi kufikia hoteli za kifahari za aina tofauti 25 zinazotoa huduma za kitalii katika nchi sita za Afrika.


Alisema mbali na uwekezaji katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, pia TPS ina vitega uchumi vitega uchumi 10 katika nchi za Afghanistan, Pakistan na Tajikistan.


Serena Hotels zilianzishwa Tanzania mnamo mwaka 1996 zikianza na vituo 5 na kupanuka hadi
10 uwekezaji ukiwa Arusha, Ukanda wa Kaskazini wa Utalii, Ukanda wa Kusini wa Utalii na sasa Dar es salaam.

0 comments

Post a Comment