Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - Mkuu wa Polisi wa Uingereza ajiuzulu kwa Ufisadi

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Mkuu wa polisi nchini Uingereza ajiuzulu
Mkuu wa polisi nchini Uingereza, Sir Paul Stephenson, amejiuzulu -- akiwa mhanga wa hivi karibuni kabisa katika kashfa ya udakuzi wa simu za watu na madai ya ufisadi yanayowahusisha waandishi wa habari wa shirika la magazeti ya Uingereza linalomilikiwa na tajiri Rupert Murdoch.


Sir Paul alisema anajiuzulu kutokana na shutma juu ya uhusiano kati ya polisi na shirika la News International.


Alikanusha kutenda kosa lolote, haswa katika suala la kumwajiri mwandishi wa zamani wa shirika la News International , ambaye alitiwa mbaroni wiki iliyopita.


Polisi imekiri kufanya kosa katika juhudi zao za siku za nyuma kuchunguza udakuzi wa simu.Pia wameshtumiwa kupokea fedha kutoka kwa waandishi wa habari.


Wakati huo huo mapema siku ya Jumapili, mmoja wa maafisa waandamizi wa Bw Murdoch, Rebekah Brooks, alitiwa mbaroni mjini London kwa tuhma za udakuzi wa simu za watu na ufisadi.


Baadaye ameachiliwa huru kwa dhamana.


Bi Brooks, ambaye alikuwa mhariri wa gazeti linalohusishwa na kashfa ya udakuzi wa simu, wakati ambapo makosa mengi yanadaiwa kutendeka, amekanusha kujua lolote kuhusu madai hayo.

0 comments

Post a Comment