Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja, Naibu wake Mh. Adama Malima (kulia) na Katibu Mkuu wake Bw. David Jairo, katika moja ya mikutano mingi na wanahabari kuelezea mstakabali wa hali ya umeme nchini
BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI ILIYOWASILISHWA NA WAZIRI WILLIAM NGELEJA LEO HUKO BUNGENI DODOMA IMEKATALIWA NA WAHE. WABUNGE NA WAZIRI MKUU MHE. MIZENGO PINDA AMEOMBA SERIKALI IPEWE WIKI TATU KUIREKEBISHA NA KUIRUDISHA ISOMWE UPYA.
HII NI MARA YA KWANZA KATIKA HISTORIA YA BUNGE LA NCHI HATUA HII KUFIKIWA, INGAWA HUKO NYUMA BAJETI KAMA MBILI ZILIONDOLEWA KABLA YA KUSOMWA
SPIKA WA BUNGE MHE. ANNE MAKINDA AMEAFIKI KUKATALIWA KWA BAJETI HIYO AKIITA NI NYETI NA KUSEMA ITAPOKUJA KUSOMWA TENA IWE NA MAJIBU YA UHALISIA NA MIPANGO INAYOTEKELEZEKA, KWA KUZINGATIA ATHARI AMBAZO WANANCHI NA NCHI YENYEWE INAPATA KUTOKANA NA UKOSEFU WA UMEME.
WENGI WALITEGEMEA KWAMBA WAZIRI NGELEJA KUKAANGWA ILE MBAYA, ILA SIO KUKATALIWA KWA BAJETI NZIMA NA KUTAKIWA IANDIKWE UPYA ILI KIELEWEKE.
----------------------------------------
Wakati huo huo Mhe. Pinda amekuja juu Bungeni na kusema amekasirishwa sana na barua inayosemekana imeandikwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. David Jairo ikiwataka maofisa wa Wizara hiyo kuchangia Sh. 50M/- kila idara ili hotuba ya bajeti ipite.
Barua hiyo, iliyoandikwa kwa maofisa ambao majina yao yako kapuni, iliibuliwa na Mbunge wa Kilindi, Mh. Beatrice Shelikindo, na akauliza hizo pesa zingetumika vipi na kwamba ziliagiwa zipelekwe kwenye akaunti ya Geological Survey of Tanzania (GST) benki ya NMB tawi la Dodoma.
Waziri Mkuu aliliambia Bunge kwamba kama anmri ingekuwa yake angemfukuza kazi Bw. Jairo hapo hapo na kusema kitendo alichokifanya kilistahili adhabu hiyo. Ila alisema kwa vike Rais ndiye mwenye mamlaka ya kumtimua Bw. Jairo atasubiri akipata nafasi ya kuongea nae na kumuomba afanye hivyo.
“Mheshimiwa Rais Kikwete yuko ndami ya ndege hivi sasa akielekea Pretoria, Afrika ya Kusini, hivyo simpati kwa simu ila nitampigia mara tu baada ya kutua na kutulia.
“Kwa manufaa ya Taifa nitamshauri Rais amfukuze kazi Jairo”, alisema huku wabunge wa kambi zote wakimshangilia kwa nguvu.
0 comments