Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - Gaddafi aibuka tena na kutoa ujumbe kwa mahasimu wake

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi ametoa ujumbe wa sauti katika televisheni ya nchi hiyo, ukieleza kwamba atafanya jitihada zake zote katika kuwakomboa wananchi wa nchi hiyo dhidi ya mahasimu wake.


Ujumbe huo ulisikilizwa na maelfu ya wafuasi wake waliokusanyika katika mji wa Al-Ajaylat, ambao upo umbali wa kilometa 80 magharibi mwa Tripoli.


Safari hii, Gaddafi amemwita rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ambae ni muungaji mkono wa mwanzo kabisa wa kampeni ya kuzuia ndege kuruka kwa lengo la kuwalinda raia wa Libya na majeshi yake kuwa ni mhalifu wa kivita.


Akizungumza kwa sauti, kiongozi hiyo alisema " Mwisho wa NATO utakuwa Libya... Mwisho wa Umoja wa Ulaya utakuwa katika mapigano haya"


Kiasi ya umbali wa kilometa 100, upande wa magharibi mwa mji wa Tripoli, ambayo ndiyo ngome ya Gaddafi, katika kijiji cha Al-Qawalish wapiganaji waasi wanasema wanakusanya nguvu ili waweze kusonga mbele kuelekea mashariki mwa mji wa Garyan.


Kwa mujibu wa makamanda wa operesheni hiyo, hatua hiyo itawawezesha kuidhibiti barabara kubwa inayoelekea mji mkuu, Tripoli. Lakini siku moja kabla wanajeshi watiifu kwa Gaddafi walifanya mashambulizi ya kushtukiza dhidi ya waasi hao katika mji wa Al-Qawalish na kusababisha vifo vya waasi 7.


Hata hivyo kwa mujibu wa Shirika la Habari la Uingereza Reuters baadae waasi hao waliweza kurudi na kuonekana kama wanadhibiti tena kijiji hicho.


Mapigano yakiendelea nchini Libya, Uingereza imesema itatoa ndege nyingine nne za kivita ili kuweza kuungeza nguvu katika operesheni inayoongozwa na NATO nchini humo.


Ongezeko hilo litaifanya idadi ya ndege za kivita zilizotolewa na nchi hiyo kuwa 16 badala ya zile 12 ambazo kwa hivi sasa zipo katika uwanja wa mapambano.


Akitoa kauli hiyo sambamba na mkutano wa kundi la mataifa ya mashauriono kuhusu Libya, Waziri katika Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Uingereza, Alistair Burt amesema ndege hizo ni mahususi katika kukagua na kutambua.


Jana, Katibu Mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmusses alitoa wito kwa wanachama wa jumuiya hiyo kuchangia zaidi ndege kwa lengo la kuyaangamiza majeshi ya Gaddafi kwa shabaha ya kuwalinda raia wa Libya na kuzuia ndege kuruka nchini humo.


Mkutano wa kundi la nchi zinazoshauriana kuhusu Libya tayari umeshaanza mjini Istanbul - Uturuki. Lengo ni kutafuta suluhu ya kisiasa nchini humo,kwa kumshinikiza Gaddafi kuondoka madarakani ili kuepusha mgogoro huo usiendelee bila ya kikomo.

0 comments

Post a Comment