IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Rais Barack Obama wa Marekani anawahimiza wabunge wa nchi hiyo kuepusha maafa makubwa, kwa kufikia makubaliano kwa haraka, ili Marekani isijekushindwa kulipa madeni yake, mwanzoni mwa mwezi wa Agosti.
Akizungumza katika Ikulu ya Marekani, huku wabunge wa vyama vya Demokratik na Republikan, wakikutana mbali mbali kutafuta ufumbuzi, Obama alionya kuwa hawana muda mrefu. Viongozi wa Seneti vile vile wanajaribu kuafikiana kabla ya kufikia tarehe 2 Agosti.
Mwenyekiti wa Benki Kuu ya Marekani, Ben Bernanke ameonya juu ya athari za kutopata makubaliano ya kupandisha kiwango cha deni la Marekani, ambalo hivi sasa ni dola trilioni 14.3. Amesema hiyo huenda ikaathiri uchumi katika kila pembe ya dunia.
You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - Marekani inadaiwa dola trilioni 14.3, Obama aomba wabunge warithie ongezeko la deni
0 comments