Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - UDSM, NSSF zasaini mkataba wa ardhi

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
CHUO Kikuu cha Dar es Salaam, na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), zimetiliana saini mkataba wa kutoa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya magonjwa ya moyo, katika maeneo ya Mlimani City.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhan Dau, alisema makubaliano hayo yamekuja baada ya Serikali za Tanzania na India, kukubalina kuhusu ujenzi wa  hospitali hiyo, kupitia Tasisi ya Magonjwa ya Moyo Apollo ya India.

Alisema katika makubaliano hayo, serikali ilisema chuo kikuu, kitatoa ardhi itakayotumika kujenga hospitali hiyo.Mkataba wa kutoa ardhi hiyo, ulisainiwa jana na kwa mujibu wa Dk Dau, ujenzi utaanza baada ya kuanza kwa mwaka ujao wa fedha.

Mkurugenzi huyo alisema  NSSF, itatoa fedha za ujenzi wa hospitali na serikali ya India, itato vifaa vyote vya huduma na wataalamu wa maradhi ya moyo.Alisema baadhi ya wataalamu wa hapa nchini wataondoka wiki hii kwenda India katika kitengo cha usanifu wa majengo ili kupata uzoefu.

"Si tunajua kuwa serikali ilikuwa inatumia fedha nyingi kupeleka wagonjwa wa moyo nje ya nchi, lakini mpango huu utaipunguzia gharama hizo serikali maana wagonjwa wote watakuwa wanatibiwa hapa hapa,"alisema Dk Dau.

Alisema serikali imekuwa ikitumia wastani wa Dola milioni 8 hadi 9, kwa ajili ya kuwapeleka wagonjwa moyo, nje ya nchi na kwamba fedha hizo zingekuwa zinafanya mambo mengine ya maendeleo ya nchi.

"Kwa upande wetu fedha zipo za kutosha na tukianza hakuna kusimama na bahati nzuri kama mnavyoona tayari tumesaini mkataba wa makubaliano ya kupata ardhi,"alisema Dk Dau.

Alisema kuwa ujenzi wa hospitali hiyo utadumu kwa kati ya miezi 18 na 20 .

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam (Taaluma), Profesa Makenya, alielezea kufarijika kwake juu ya kuanzishwa kwa ujenzi wa hospitali hiyo na kwamba katika majengo hayo kuna sehemu watatoa shahada ya uzamivu katika fani ya afya.

0 comments

Post a Comment